Home Kimataifa Kenya yaandaa kongamano la Umoja wa Afrika la katikati ya mwaka

Kenya yaandaa kongamano la Umoja wa Afrika la katikati ya mwaka

0
kra

Awamu ya 5 ya kongamano la katikati ya mwaka la ushirikiano baina ya Umoja wa Afrika, AU na mashirika ya kikanda ya kiuchumi unaandaliwa leo Jumapili huko Gigiri, kaunti ya Nairobi.

Mkutano huo ulianza saa nne unusu asubuhi.

kra

Mandhari ya mwaka huu ni “Kuharakisha kuafikiwa kwa eneo la biashara huru barani Afrika” Wakuu wa nchi na serikali 12 wanahudhuria mkutano huo ambapo wengi kati yao waliwasili Nairobi Jumamosi jioni.

Waziri wa mambo ya nje Alfred Mutua ana imani kwamna mkutano huu utafanikiwa pakubwa.

Kongamano la katikati ya mwaka la ushirikiano baina ya Umoja wa Afrika na mashirika ya kikanda ya kiuchumi lilianzishwa mwaka 2017 ili kuleta pamoja mashirika mbali mbali ya kikanda ya kibiashara na umoja wa Afrika ili kuratibu kazi zao na kushirikiana kuhakikisha utekelezaji wa ajenda ya kuunganisha nchi za bara hili na lilichukua mahala pa mikutano ya miezi ya Juni na Julai.

Majukumu ya kikao hicho ni pamoja na kutathmini ufanisi wa ajenda ya kuunganisha bara Afrika na kuratibu mbinu za kuharakisha kuafikiwa kwa ajenda hiyo.

Kongamano hilo pia limejukumiwa kuhakikisha kwamba kila shirika linatekeleza majukumu tofauti na wala sio majukumu sawia.