Home Habari Kuu Kenya yaadhimisha siku kuu ya Mashujaa

Kenya yaadhimisha siku kuu ya Mashujaa

0
Maadhimisho ya siku kuu ya Mashujaa katika uwanja wa Kericho Green.

Rais William Ruto Leo Ijumaa ataongoza wakenya kuadhimisha sherehe za mwaka huu za Mashujaa katika kaunti ya Kericho.

Sherehe za mwaka huu ni za 60, na zitaandaliwa katika uwanja wa michezo wa Kericho green.

Siku kuu ya Mashujaa  huandaliwa kila mwaka kuwakumbuka Mashujaa waliopigania uhuru wa taifa hili.

Hapo awali siku hii ilijulikana Kenyatta day, lakini jina hilo lilibadilishwa wakati katiba mpya iliporasimishwa.

Wakati wa sherehe hizi, watu mbalimbali hutuzwa kama Mashujaa kutokana na wajibu muhimu waliotekeleza katika kukuza maendeleo ya taifa hili.

Milango katika uwanja wa Kericho green ilifunguliwa saa tisa asubuhi, kuwaruhusu wakenya kuingia, lakini milango hiyo ilifungwa saa mbili asubuhi baada ya uwanja huo kujaa.

Website | + posts