Home Michezo Kenya wazimwa nyumbani na Uganda fainali ya CECAFA

Kenya wazimwa nyumbani na Uganda fainali ya CECAFA

0

Wenyeji Kenya waligutushwa baada ya Uganda kutoka nyuma na kuwacharaza mabao 2-1,kwenye fainali ya kombe la CECAFA  kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 18, iliyosakatwa Ijumaa katika uwanja wa Jomo Kenyatta Mamboleo  kaunti ya Kisumu.

Cyprus Owuor  alifungua ukurasa wa Kenya kwa bao la kwnza kunako kipindi cha pili kabla ya Batiibwe Okelo kukomboa  bao hilo dakika 12,kabla ya kipenga cha mwisho  na kulazimu mchuano kuamuliwa  kupitia penati.

Ililazimu dakika 30 kuongezwa ili kutengamisha majimbi hao  lakink punde tu baada ya sekunde 50 za nyongeza,  Hakim  Mutebi alicheka na nyavu kwa goli la ushindi.

Uganda walituzwa shilingi milioni 2 nukta 4 kwa ubingwa huo huku Kenya waliokuwa hawajashinfwa mechi wakiridhia medali ya fedha.

Tanzania ilimaliza ya tatu baada ya kuwazidia maarufa Rwanda mabao 3-1 katika mchuano wa  afasi ya tatu na nne.