Home Biashara Kenya, Toyota kushirikiana kuchochea sekta ya utengenezaji magari nchini

Kenya, Toyota kushirikiana kuchochea sekta ya utengenezaji magari nchini

0
kra

Kenya na kampuni ya Toyota Tsusho ya Japani zimetia saini mpangokazi wa makubaliano ya kushirikiana katika utengenezaj wa magari na uendelezaji wa nishati mbadala. 

Kutokana na makubaliano hayo, kampuni ya Toyota itaanzisha kiwanda cha kutengeneza magari humu nchini. Mwanzoni, kampuni hiyo imeahidi kuwekeza shilingi milioni 800 katika kampuni za utengenezaji magari mjini Thika.

kra

Rais William Ruto amesema hatua hiyo itapiga jeki sekta ya viwanda nchini Kenya, kuimarisha uhusiano kati ya Kenya na Japani na kupanua nafasi za ajira kwa Wakenya.

Alisema lengo ni kuhakikisha magari yanayotengenezwa humu nchini ni ya gharama nafuu na hivyo kuwakatisha tamaa watu kununua magari ambayo tayari yametumika.

“Lazima tuwe na uwiano kati ya idadi ya magari yanayoagizwa na magari mapya yanayotengenezwa,” alisema Rais Ruto.

Akiwa jijini Tokyo nchini Japani, Ruto alishuhudia kutiwa saini kwa makubaliano hayo mbele ya Rais wa kampuni ya Toyota Tsusho ya Japani, Ichiro Kashitani.

Kuhusiana na uendelezaji wa nishati mbadala, makubaliano hayo yalijumuisha shilingi bilioni 15 za Nishati ya Kilimo cha Upepo, shilingi bilioni 8 za Nishati ya Jua ya Isiolo na shilingi bilioni 75 za kiwanda cha mvuke cha Menengai.