Home Biashara Kenya Power: Hitilafu ya kununua tokeni za umeme imetatuliwa

Kenya Power: Hitilafu ya kununua tokeni za umeme imetatuliwa

0

Kampuni ya Kenya Power, KP inasema hitilafu iliyokuwepo kwenye mfumo wake wa kununua tokeni za umeme imeshughulikiwa.  

Hii ina maana kuwa Wakenya sasa wanaweza wakanunua tokeni za umeme bila nuksi ya aina yoyote.

“Tuna furaha kutangaza kuwa hitilafu iliyokuwepo kwenye mfumo wetu wa kununua tokeni za umeme imetatuliwa na wateja sasa wanaweza wakanunua tokeni hizo,” imesema kampuni ya Kenya Power katika taarifa.

Awali, hitilafu hiyo iliwaathiri Wakenya waliojaribu kununua tokeni za umeme bila mafanikio.

“Tunakumbana na hitilafu kwenye mfumo wetu wa kulipia umeme ambayo inaathiri ununuaji wa tokeni za umeme,” ilitangaza Kenya Power wakati huo.

“Tunafanya kazi kurejesha hali ya kawaida haraka iwezekanavyo. Tunaomba radhi kutokana na usumbufu uliosababishwa na hali hiyo.”