Timu ya taifa ya soka Harambee Stars imeambulia sare tasa na Zimbabwe katika mchuano wa kwanza wa kundi J, kufuzu kwa fainali za AFCON uliosakatwa Ijumaa jioni katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Kampala,Uganda.
Timu zote zilibuni nafasi haba za kufunga mabao huku zikiwa na ubutu mwingi.
Kenya ililazimika kuchezea ugenini nchini Uganda kutokana na kukosa uwanja humu nchini kwa sasa,viwanja wa Kasarani na Nyayo vikikarabatiwa.
Harambee Stars itaondoka kesho kuelekea Afrika Kusini ambapo watachuana na Namibia Jumanne ijayo kwa mchuano wa pili.
Vijana wa kocha Engin Firat walilazimika kucheza bila huduma za nahodha na mshambulizi Michael Olunga anayeuguza jeraha.