Home Biashara Kenya na Uganda zashirikiana kuimarisha utalii

Kenya na Uganda zashirikiana kuimarisha utalii

Ongezeko la matangazo kuhusu maeneo ya utalii katika nchi hizi mbili, litasaidia pakubwa kuongeza idadi ya watalii wanaozuru nchi hizo mbili za Afrika Mashariki.

0

Kenya na Uganda zinajadiliana kuhusu mbinu za kutafuta soko la bidhaa za utalii, ili kuongeza idadi ya watalii wanaozuru nchi hizi mbili.

Ongezeko la matangazo kuhusu maeneo ya utalii katika nchi hizi mbili, litasaidia pakubwa kuongeza idadi ya watalii wanaozuru nchi hizo mbili za Afrika Mashariki.

“Idadi kubwa ya watu, wakiwemo washika dau katika sekta ya utalii, hawafahamu bidhaa za kitalii katika nchi jirani, huku mataifa hayo mawili yakiwa soko tayari la kitalii,” alisema John Mulimba, Waziri wa mambo ya nje wa Uganda.

Akizungumza katika kongamano la pili kuhusu utalii baina ya Kenya na Uganda katika kaunti ya Kwale, Mulimba alisema nchi hizo mbili zina na uwezo mkubwa wa kitalii, wakuongeza idadi ya watalii.

“Tunaweza ongeza idadi ya wakenya 370,000 waliozuru Uganda na raia 150,000 wa Uganda waliozuru Kenya mwaka jana. Tunapaswa kuhakikisha ushirikiano huu unafanya kazi,” aliongeza Mulimba.

Wengi wa wakenya waliozuru Uganda mwaka jana, walikuwa wakishiriki shughuli za michezo, na tamasha za muziki.

Kenya inalenga kupigia debe fuo za changarawe, mbuga za wanyama na uogeleaji wa baharini miongoni mwa bidhaa zingine za kitalii, huku Uganda ikilenga kupigia debe Milima yake iliyo na Sokwe, Simba wanaokwea miti na zaidi ya aina 1063 ya ndege kwa watalii wanaotoka Kenya.

Website | + posts