Home Habari Kuu Kenya na Marekani kujenga barabara kuu ya Nairobi hadi Mombasa

Kenya na Marekani kujenga barabara kuu ya Nairobi hadi Mombasa

0

Kenya imetia sahini ya ushirikiano na taifa la Marekani katika ujenzi wa barabara kuu ya kutoka Nairobi hadi Mombasa.

Barabara hiyo yenye Leni/njia nne hadi sita kila upande, na yenye umbali wa takribani kilomita 440, itagarimu dola bilioni 3.6 sawa na shilingi bilioni 471 za Kenya.

Ufadhili wa mradi huo utatoka kwa wawekezaji wa Kimataifa, mashirika ya maendeleo duniani, wawekezaji wa kibinafsi wa hapa nchini na hazina ya malipo ya uzeeni.

Ujenzi wa barabara hiyo umekuwa ndoto ya viongozi wengi waliopita na sasa huenda ikatimizwa na rais William Ruto na kuwapa wakenya afueni hasa wanaotumia kwa safari za abiria na mizigo.

Vile vile, Kenya pia imeagiza magari 150 ya kivita aina ya M1117 yatakayo letwa nchini mwezi Septemba mwaka huu.

Taarifa hizi nzuri zinajiri wakati rais Ruto yumo nchini Marekani Kwa ziara ya Kitaifa huku wakenya wakijawa na matumaini chungu nzima kuwa safari hiyo italeta manufaa mengi nchini.

Boniface Musotsi
+ posts