Home Habari Kuu Kenya na Guinea-Bissau kuimarisha biashara baina yazo

Kenya na Guinea-Bissau kuimarisha biashara baina yazo

Rais Ruto alisema atashinikiza kuanzishwa kwa safari za moja kwa moja kati ya Kenya na Guinea-Bissau.

0
Rais William Ruto (Kushoto) na mwenzake wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embaló (Kulia).

Kenya na Guinea-Bissau zimeazimia kutekeleza sera zitakazoimarisha biashara baina ya mataifa hayo mawili.

Rais William Ruto, alisema kwa sasa kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili ni cha chini, lakini kuna fursa kuimarisha hali hiyo.

Kiongozi wa taifa alisema  Kenya na Guinea-Bissauz ziko makini kutekeleza mkataba wa maelewano, uliobuni tume ya pamoja ya ushirikiano JCC, na kutiwa saini mwaka 2022.

Rais Ruto alidokeza kuwa ushirikiano wa sekta za kibinafsi kati ya nchi hizo mbili, utaongeza viwango vya biashara kati ya nchi hizo mbili.

Aliyasema hayo leo Ijumaa wakati wa mkutano na wanahabari, baada ya kushiriki mazungumzo na mwenyeji wake Rais Umaro Sissoco Embalo.

Rais Ruto ambaye yuko kwa ziara ya kiserikali nchini Guinea Bissau, alitunukiwa tuzo ya juu zaidi nchini humo na Rais Embalo katika ikulu ya Rais.

Wakati huo huo, Rais Ruto alisema atashinikiza kuanzishwa kwa safari za moja kwa moja kati ya Kenya na Guinea-Bissau.

Website | + posts