Home Biashara Kenya na Ghana zasaini mikataba ya biashara

Kenya na Ghana zasaini mikataba ya biashara

0

Kenya na Ghana zimetia saini Mikataba ya Maelewano, MoU inayodhamiria kukuza ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili. 

Mikataba hiyo mitatu muhimu ilitiwa saini wakati wa kongamano la biashara lililofanyika mjini Accra nchini Ghana.

“Utiaji saini wa mikataba hiyo siyo tu kwamba inaashiria kujitolea kwetu kwa pamoja kuchochea ukuaji endelevu na ustawi wa pande mbili nchini Kenya na Ghana, bali pia unaashiria ari ya ushirikiano kati ya sekta ya kibinafsi na serikali kwa manufaa ya watu,” amesema Waziri wa Biashara wa Kenya Rebecca Miano.

Miano ni miongoni mwa viongozi walioandamana na Rais William Ruto katika ziara yake ya siku tatu nchini Ghana.

 

 

Website | + posts