Rais William Ruto amesema uhusiano baina ya Kenya na China ni imara, na ambao umebadilisha miundombinu ya barabara, reli na bandari za hapa nchini.
Rais alidokeza kuwa ushirikiano huo umewanufaisha pakubwa raia WA nchi hizo mbili.
Akizungumzia manufaa ya ushirikiano huo, Rais Ruto alitaka ujenzi wa miundomsingi kama vile reli ya kisasa ya SGR kutoka Mombasa hadi Naivasha, barabara ya Nairobi Express way na baadhi ya barabara katika maeneo ya mashinani.
Kulingana na Rais Ruto, miradi hiyo imeifanya Kenya kuwa kitovu cha usafiri sio tu katika Kanda ya Afrika Mashariki, lakini katika bara mzima kwa jumla.
Rais alielezea kuhusu mkutano wake na Rais wa China Xi Jinping Jijini Beijing, kabla ya mkutano baina ya China na mataifa ya bara Afrika (FOCAC).
Wakati wa mkutano huo, Rais Xi agreed alikubali bidhaa za kilimo kutoka Kenya kuingia katika soko la China, hatua ambayo Rais Ruto alisema itapiga jeki uuzaji wa mazao kutoka Kenya.
Viongozi hao wawili walikubaliana kuendeleza miradi ya miundomsingi katika Kanda hii, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa reli ya kisasa ya SGR, ujenzi wa barabara ya Rironi-Mau Summit-Malaba, ambayo itaungaisha Kanda hii.