Home Michezo Kenya kuzindua uhasama wa jadi na Uganda fainali ya CECAFA kwa makinda

Kenya kuzindua uhasama wa jadi na Uganda fainali ya CECAFA kwa makinda

0

Timu ya taifa ya Kenya ya soka kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 18, itazindua uhasama wa tangu jadi dhidi ya Uganda kwenye fainali ya mashindano ya kuwania kombe la CECAFA, Ijumaa Alasiri katika uwanja wa Jomo Kenyatta kaunti ya Kisumu.

Kenya iliyokuwa imeshinda mechi zote za kundi A dhidi ya Rwanda bao 1-0,ikaititiga Sudan magoli 5 kwa bila na kuwacharaza Somalia mabao 4-1 na kuongoza kundi A kwa alam 9.

Katika semi fainali Junior Stars wanaofunzwa na kocha Salim Babu, waliibandua Tanzania kupitia penati kufuatia sare tasa kabla ya kutinga fainali ya Ijumaa.

Uganda nao walipoteza mechi ya kwanza dhidi ya Tanzania bao 1 kwa bila, kabla ya kuishinda Zanzibar bao 1 kwa nunge na kuilaza Sudan Kusini magoli mawili kwa bila na kumaliza ya kwanza kundini B kwa pointi 6.

Katika semi fainali Uganda iliwabandua Rwanda kupitia kwa bao la utata.

Fainali hiyo itaanza saa nane unusu ikitanguliwa ne mechi ya kusaka mshindi wa tatu baina ya Rwanda na Tanzania.

Website | + posts