Home Biashara Kenya kutumia kikamilifu mabasi ya umeme kufikia mwaka 2027

Kenya kutumia kikamilifu mabasi ya umeme kufikia mwaka 2027

0
Kenya kutumia mabasi ya umeme kikamilifu kufikia mwaka 2027.

Waziri wa ustawi wa viwanda Rebecca Miano, amesema kuwa taifa hili linatarajiwa kutumia kikamilifu mabasi yanayotumia nguvu za umeme kufikia mwaka 2027.

Kulingana na Miano, hatua hiyo inaambatana na ajenda ya serikali yakufanya mageuzi katika sekta ya uchukuzi, kupitia kupunguza utoaji hewa ya kaboni kwa lengo kukabiliana na mabadiliko ya ya hali tabia nchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabasi ya kwanza yanayotumia umeme ambayo yametengenezewa hapa nchini na kampuni ya BasiGo kwa ushirikiano na kampuni ya Kenya ya utengenezaji magari KVM, waziri huyo pia alizindua sera ya uchukuzi wa kitaifa kupitia nguvu za umeme, ili kuanzisha mchakato huo.

Alisema sera hiyo inapendekeza kuanzishwa kwa vishawishi vitakavyopiga jeki ununuzi wa mabasi yanayotumia umeme, ikiwa ni pamoja na kupunguza ushuru wa magari hayo hadi asilimia 10, sawia na ilivyo katika sheria ya fedha ya mwaka 2023.

”Serikali inatambua wajibu mkubwa unaotekelezwa na uwekezaji wa  BasiGo katika ukuaji wa uchumi wa taifa kubuni nafasi za ajira na kuimarisha maisha ya wananchi wetu. Tumebuni mazingira bora ya uwekezaji, sera dhabiti pamoja kulainisha sheria zinazonuia kuwavutia wawekezaji,”alisema waziri huyo.

Baadhi ya mabasi yaliyozinduliwa yanayotumia umeme, yatatumiwa na kampuni za Cito Hoppa na Super Metro.

Website | + posts