Home Kimataifa Kenya kupokea dozi 50,000 za chanjo ya Mpox

Kenya kupokea dozi 50,000 za chanjo ya Mpox

Ugonjwa wa Mpox umeripotiwa katika mataifa manne ya Afrika tangu mwezi Julai mwaka huu yakiwa ni Kenya, Burundi, DRC na Rwanda.

0
kra

Kenya inatarajia kupokea dozi 50,000 za chanjo ya ugonjwa wa Mpox kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ushirikiano na serikali ya Marekani.

Kenya ni mojawapo wa mataifa matano ya Afrika yaliyolengwa kupokea msaada wa chanjo hiyo kama njia ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.

kra

Mataifa mengine yatakayopokea chanjo hiyo ya msaada ni Jamhuri ya Kidemkorasia ya Congo (DRC), Burundi, Rwanda na Uganda.

Hii inafuatia hatua ya WHO kutangaza ugonjwa wa Mpox kuwa ugonjwa wa dharura ya afya ya umma duniani.

Awali, hatua sawia ilitangazwa na Kituo Cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa barani Afrika cha Africa CDC.

Ugonjwa wa Mpox umeripotiwa katika mataifa manne ya Afrika tangu Julai mwaka huu yakiwa ni Kenya, Burundi, DRC na Rwanda.

Kando na Afrika, mataifa ya Uswidi na Pakistan pia yamenakili visa vya kwanza vya ugonjwa huo, huku Afrika ikiripoti visa 14,000 na kusababisha vifo 456 katika nchi 15.

Mpox ni ugonjwa unaoambukiza kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu, na pia kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa kuvalia nguo ya mgonjwa, vyombo vya kula chakula na pia kupitia tendo la ndoa.

Website | + posts