Home Kimataifa Kenya kuandaa mkutano kuhusu maswala ya mipakani kaunti ya Mandera

Kenya kuandaa mkutano kuhusu maswala ya mipakani kaunti ya Mandera

0
kra

Kenya inaandaa mkutano wa siku mbili, utakaoshughulikia masuala ya mpakani ambapo wajumbe kutoka Kenya, Somalia na Ethiopia, watahudhuria katika kaunti ya Mandera.

Mkutano huo kwa jina “Mandera Cluster”, unanuia kushughulikia masuala kadhaa na kuimarisha ushirikiano miongoni mwa jamii za mataifa haya matatu.

kra

Kiini cha mkutano huo ni mpango wa kuimarisha ustahimilivu katika mipaka ya jamii iliyobuniwa ili kuimarisha ustahimilivu na kupunguza utegemezi wa usaidizi wa kibinadamu miongoni mwa jamii za mipakani.

Mpango huo unasisitiza kukuza umiliki wa ndani kwa kusaidia uongozi katika kupanga, kutekeleza na ufuatiliaji wa uwekezaji wa maendeleo.

Naibu kamishna wa Kaunti ya Mandera, Patrick Meso, aliwashukuru waandalizi kwa kutekeleza hatua za usalama kwa wafanyabiashara wanaovuka mipaka.

Alihimiza kuishi pamoja kwa amani miongoni mwa jamii husika.

Abdi-Rashid Abdi Hassan, kamishna wa wilaya ya Beled-Hawa nchini Somalia, aliahidi kupigania mipango ya ustahimilivu, ikiwa ni pamoja na mipango ya kilimo na ufugaji ili kukuza kutegemeana miongoni mwa wakazi.

Website | + posts