Home Kimataifa Kenya kuandaa kipute cha CHAN mwaka 2024

Kenya kuandaa kipute cha CHAN mwaka 2024

0
kra

Kenya imeteuliwa kuandaa fainali za kombe la Afrika kwa wanandinga wanaopiga soka katika ligi za nyumbani mwaka 2024.

Makala hayo ya tisa yanatarajiwa kuandaliwa mwezi Septemba.

kra

Kenya iliteuliwa kuwa mwenyeji wa michuano ya CHAN mwaka 2018 lakini ikapokonywa michuani hiyo iliyopelekwa nchini Morocco kutokana na utepetevu wa maandalizi.

Kenya itatumia michuano ya mwaka ujao kujitayarisha kuandaa kipute cha AFCON mwaka 2027 pamoja na Uganda na Tanzania.