Kenya imekariri kujitolea kumaliza ugonjwa wa kifua kikuu nchini.
Haya yamesemwa Alhamisi na Katibu katika Wizara ya Afya ya Umma Mary Muthioni, alipokuwa akihutubua kikao cha nne cha Afrika kuhusu kifua kikuu katika kaunti ya Nairobi.
Kulingana na Muthoni, mikakati iliyowekwa kukabiliana na ugonjwa huo imefanikiwa na kupita viwango vilivyokisiwa.
“Kenya ndio nchi ya kwanza kutekeleza na kutumia dawa za kutibu kifua kikuu zilizo salama kwa watoto na zile kutibu ugonjwa wa kifua kikuu,” alisema Muthoni.
Kenya pia imenakili kupungua kwa visa vya kifua kikuu kwa asilimia 44 na kupita kiwango cha dunia cha asilimia 35.