Home Biashara Kenya imebuni mazingira bora ya biashara, asema Mvurya

Kenya imebuni mazingira bora ya biashara, asema Mvurya

Mvurya alisema serikali imeimarisha juhudi za kubuni mazingira mwafaka kwa biashara na uwekezaji hapa nchini.

0
Waziri wa biashara Salim Mvurya (kushoto) na mwenzake wa Fedha John Mbadi (Kulia), katika kaunti ya Kwale.
kra

Waziri wa uwekezaji, biashara na viwanda Salim Mvurya, leo Ijumaa aliungana na mwenzake wa Fedha John Mbadi, kuhudhuria kongamano la 24 dhidi ya ulalungi wa pesa, linalowaleta pamoja mawaziri kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika.

Mkutano huo ulioandaliwa Diani kaunti ya Kwale, ambao unawajumuisha mawaziri 21, unalenga kujadili sheria na masharti yanayolenga kukabiliana na ulanguzi wa pesa na ufadhili wa ugaidi.

kra

Akizungumza katika mkutano huo, Mvurya alisema serikali imeimarisha juhudi za kubuni mazingira mwafaka kwa biashara na uwekezaji hapa nchini.

“Serikali imeweka mikakati bora kuchochea biashara. Ulanguzi wa pesa na ugaidi, ni maswala tunapaswa kukabiliana nayo vilivyo kama taifa na kama bara,” alisema Mvurya.

Aliongeza kuwa kongamano hilo limejiri wakati mwafaka, kwani linaangazia pengo zilizopo katika kukabiliana na ulanguzi wa fedha kama taifa na katika bara lote la Afrika.

Website | + posts