Waziri wa Michezo Kipchumba Murkomen ametoa hakikisho la Kenya kuwa tayari kuandaa mashindano ya uendeshaji baiskeli barani Afrika kati ya tarehe 8 na 13 mwezi ujao katika kaunti za Elgeyo Marakwet na Uasin Gishu.
Waziri alizungumza haya leo alipohudhuria uzinduzi wake jijini Nairobi, akijivunia Kenya kupokezwa maandalizi kwa mara ya kwanza.
“Kenya tunajivunia michezo na haya mashindano yatatupa fursa ya kudhihirisha uwezo wa taifa letu kuandaa mashindano ya kimataifa.”akasema Murkomen
Kwa upande wake waziri wa michezo wa Elgeyo Marakwet Purity Koima, ameelezea matumaini yake ya kuandaa mashidnano ya kufana, akisema yataitangaza vyema kaunti hiyo kama kituo bora kwa watalii.