Home Kaunti Kenya haijanakili kisa kipya cha ugonjwa wa Mpox

Kenya haijanakili kisa kipya cha ugonjwa wa Mpox

Wizara hiyo ilisema kuwa inachunguza sampuli 33 katika kaunti za Busia, Mombasa, Nairobi na Nakuru.

0
kra

Taifa hili halijanakili kisa chochote kipya cha ugonjwa wa Mpox, katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kulingana na taarifa ya wizara ya afya, idadi ya visa vya ugonjwa huo vilivyothibitishwa hapa nchini, inasalia kuwa tano, ambapo kaunti za  Taita Taveta, Busia, Nairobi, Mombasa na Nakuru zikinakili kisa kimoja kila kaunti.

kra

Wizara hiyo ilisema kuwa inachunguza sampuli 33 katika kaunti za Busia, Mombasa, Nairobi na Nakuru.

Katika muda wa saa 24 zilizopita, wasafiri 9,917 wamefanyiwa uchunguzi wa ugonjwa huo, katika vituo 26 vya mpakani.

Aidha wizara hiyo ilisema zoezi la uhamasishaji wa umma unaendelea ili kukabiliana na unyanyapaa na maambukizi zaidi ya ugonjwa huo, huku uchunguzi zaidi wa Mpox, ukiendelea.

Website | + posts