Home Biashara Kenya Airways yasitisha safari za Kinsasha

Kenya Airways yasitisha safari za Kinsasha

0
kiico

Kampuni ya ndege nchini ya Kenya Airways imetangaza kusitisha safari zake za kutoka Nairobi hadi Kinsasha katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuatia kuzuiliwa kwa wafanyikazi wake wawili tarehe 19 mwezi huu.

Mkurugenzi mkuu  wa kampuni ya KQ Allana Kilavuka alitangaza kusitishwa wa safari hizo, kufuatia hatua ya mamlaka ya usalama mjini Kinsasha kuendelea kuwazuia wafanyikazi wake wawili.

Kilavuka amesema wamechukua hatua hiyo baada ya kushindwa kuwakagua wafanyikazi wake wanaohudumu kutoka Nairobi hadi Kinsasha na Kinsasha hadi Nairobi.

Mzozo wa kidiplomasia unanukia kufuatia hatua hiyo baada ya DR Congo kumwita balozi wake nchini Kenya John Nyakeru.

Wahudumu hao wawili wa KQ walikamatwa kuhusiana na mzigo wa pesa taslimu wa dola milioni nane za Marekani, uliokuwa haujawekwa kwenye ndege hiyo mjini Kinsasha  bila stakabadhi maalum .

KQ katika taarifa yake ilisema haina hatia kwani wahudumu wake walikuwa wamekataa kuweka mzigo huo katika ndege yao kwa kukosa kufuata utaratibu ufaao wa kusafirisha pesa taslimu.

kiico