Home Kimataifa Kennedy Odede miongoni mwa watakaopokea tuzo ya TIME’s TIME 100,

Kennedy Odede miongoni mwa watakaopokea tuzo ya TIME’s TIME 100,

0
kra

Raia wa Kenya Dkt. Kennedy Odede ni miongoni mwa watu tajika wa bara Afrika waliochaguliwa kuwania tuzo ya  TIME’s TIME 100, itakayoandaliwa tarehe 17 mwezi Novemba Jijini Kigali nchini Rwanda.

Tuzo hiyo humtambua mtu ambaye amefanya mabadiliko ya kupigiwa mfano katika jamii.

kra

Mwanzilishi huyo wa Shining Hope for Communities (Shofco), atatuzwa katika hafla hiyo ambayo huwatambua viongozi walioleta mabadiliko katika jamii zao.

Dkt. Odede atatuzwa kutokana na wajibu muhimu uliotekelezwa na shirika la Shofco, ambalo sasa limekuwa mfano bora miongoni mwa mashirika yasiyo ya serikali kote duniani.

Shirika hilo ambalo lilianzishwa mwaka 2004 na  Dkt. Odede kama njia moja ya kuimarisha maisha ya jamii kutoka mazingira ya umaskini, shirika la Shofco sasa limebadilisha maisha ya takriban watu milioni 2.5 wanaoishi katika mitaa duni nchini Kenya.

Baada ya kuishi katika mazingira magumu ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maji safi, Odede alihakikisha bidhaa msingi zinapatikana alipozindua shirika la Shofco.

“Tulikuwa tukitembea mwendo mrefu kutafuta maji, na wakati mwingine tulipatwa na magonjwa yanayotokana na maji kwa kuwa maji tuliyoyapata hayakuwa masafi,”  alisema Dkt. Odede.

Vile vile Odede alianzisha elimu ya mtoto wa kike katika mitaa ya Kibra na Mathare, ili kuimarisha usawa wa kijinsia.

Katika shule iliyoko Kibera ambayo Ina zaidi ya  wanafunzi 500, imekuwa ilifanya mtihani wa darasa la nane KCPE 2017  huku Ile ya Mathare, ikiwa na wanafunzi 400 kuanzia shule ya chekechea hadi gredi ya saba.

Shirika hilo la Shofco pia linasaidia wanafunzi kutoka jamaa maskini katika kaunti za  Mombasa, Nakuru, Uasin Gishu na Kisii, ambao hupata zaidi ya alama 300 katika mtihani wa KCPE.

Website | + posts