Home Habari Kuu KeNHA yatakiwa kukarabati barabara ya Kisumu-Busia

KeNHA yatakiwa kukarabati barabara ya Kisumu-Busia

Otuoma  alidokeza kuwa hali ya barabara hiyo haiwezi kumudu idadi kubwa ya malori ambayo hutumia barabara hiyo kila siku.

0
Basi la abiria liligongana ana kwa ana na lori la kusafirisha mafuta eneo la Mundika, kaunti ya Busia.

Gavana wa Busia Paul Otuoma, ametoa wito kwa halmashauri ya kusimamia barabara kuu hapa nchini KeHNA, kuboresha barabara katika kaunti hiyo, ili kuzuia ajali ambazo husababishwa na barabara mbovu.

Akizungumza katika eneo la Mundika ambapo ajali kati ya lori la kubeba mafuta na basi la abiria ilitokea na kusababisha vifo vya watu wawili, Otuoma  alidokeza kuwa hali ya barabara hiyo haiwezi kumudu idadi kubwa ya malori ambayo hutumia barabara hiyo kila siku, ikizingatiawa kuwa enei hilo ni kiingilio katika Afrika ya Mashariki na kati.

“Natuma rambirambi zangu kwa familia ya waliopoteza maisha kutokana na ajali hiyo. Pia nawatakia afueni ya haraka waliojeruhiwa na ambao wanapokea matibabu katika vituo mbali mbali vya afya,” alisema Otuoma.

Wakati huo huo, Otuoma  alisema kuwa serikali ya kaunti ya itawahamasisha wakazi wake kuhusu hatua za kiusalama wakati ajali inapotokea hususan kuhusu malori ya kubeba mafuta, kutokaribia malori hayo lakini waruhusu makundi ya wataalam kutekeleza shughuli za uokoaji.

“Tuna sababu ya kushukuru kwa kuwa lori hilo halikuwa limebeba mafuta ya petroli. lingesababisha madhara makubwa kutokana na hali ya watu kutojali. Nawahimiza wakazi wa Busia kutokaribia malori ya mafuta ajali inapotokea,” alionga Gavana huyo.

Website | + posts