Home Habari Kuu KeNHA yafunga barabara za Haile Selassie na bunge ...

KeNHA yafunga barabara za Haile Selassie na bunge kwa ukarabati

0

Mamlaka ya barabara kuu nchini, KeNHA imetangaza kufunga kwa muda barabara za Haile Selassie Avenue kwenye mzunguko wa Haile Selassie pamoja na barabara ya bunge ili kupisha ukarabati wa mabomba ya maji.

Barabara hizo zitafungwa kuanzia Ijumaa saa nne usiku hadi Jumamosi saa kumi na moja alfajiri.

Wasafiri wameshauriwa kutumia njia mbadala wakati huo wa ukarabati na kushirikiana na maafisa wa trafiki.

Website | + posts