Home Habari Kuu KeNHA yafunga barabara ya Garsen -Witu

KeNHA yafunga barabara ya Garsen -Witu

0

Mamlaka ya usimamizi wa barabara kuu nchini (KeNHA) imetangaza kufunga barabara ya Garsen-Witu- hadi Lamu baada ya mto Tana kuvunja kingo zake.

KeNHA imesema mvua kubwa inayonyesha sehemu hiyo, imesababisha mafuriko makubwa ambayo yamechangia mto Tana kuvunja kingo zake.

Barabara hiyo imefungwa kati ya Gamba na Lango la Simba, huku KeNHA ikiwashauri wasafiri kutumia njia mbadala.

Website | + posts