Home Habari Kuu KeNHa kufunga mizunguko mitano ya Uhuru Highway

KeNHa kufunga mizunguko mitano ya Uhuru Highway

0

Mamlaka inayosimamia barabara kuu nchini Kenya, KeNHA imetangaza kufunga mizunguko mitano ya barabara kuu ya Uhuru kuanzia Alhamisi, Disemba 28 hadi Jumatatu, Januari mosi, mwaka 2024.

Kulingana na arifa ya KeNHA kwa umma, mizunguko hiyo mitano itafungwa ili kupisha ukarabati.

Mizunguko itakayofungwa ni pamoja na Bunyala, Nyayo Stadium, Haile Selassie Avenue, Kenyatta Avenue na University Way.

Mkurugenzi Mkuu wa KeNHA Kungu Ndungu, amewashauri watumiaji wa mizunguko itakayoathiriwa kuwa makini wanapokaribia maeneo hayo na kufuata maagizo ya maafisa wa trafiki na taa za barabarani.

Ndungu ameongeza kuwa huenda baadhi ya safu za barabara zinazoelekea kwa mizunguko hiyo zikafungwa.