Home Biashara Kenchic yaweka historia kwa kutambulika kimataifa

Kenchic yaweka historia kwa kutambulika kimataifa

0

Kampuni ya Kenchic ndio kampuni ya kwanza barani Afrika kuafiki viwango vya Baraza la Kimataifa la Ufugaji wa Kuku, IPC kwa kuhimiza upunguzaji wa matumizi ya dawa za kupambana na bakteria.

Kampuni hiyo ilitambuliwa kwa jitihada za kuhimiza ufugaji bora wa kuku.

Meneja Mkurugenzi wa Kenchic Jim Tozer ameahidi kuwa wataendelea kudumisha viwango vya ubora ili kuhakikisha usalama wa mifugo na watumiaji wa bidhaa za kuku.

Halfa hiyo iliandaliwa Jumanne na kuhudhuriwa na Katibu wa Wizara ya Mifugo Jonathan Mueke.

Mueke alikariri kuwa serikali itawasaidia wakulima kuimarisha kilimo cha ufugaji kuku.

Website | + posts