Home Kimataifa KEMRI yapokea shilingi bilioni 7 kugharamia utafiti wa chanjo ya HIV

KEMRI yapokea shilingi bilioni 7 kugharamia utafiti wa chanjo ya HIV

Taasisi ya utafiti wa matibabu nchini KEMRI imepokea ufadhili wa shillingi billioni saba za kugharamia utafiti wa chanjo ya virusi vya HIV ikishirikiana na washirika wengine wa bara la Afrika.

Ufadhili huo wa miaka mitano mkutoka kwa shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani (USAID) utawasaidia wanasayansi wa Afrika kutafuta chanjo ya virusi hivyo kwa kutumia majaribio ya awali.

Kufuatia ufadhili huo,watafiti wa KEMRI sasa wataenda katika kutafuta chanjo ya ugonjwa huo.

Maafisa wa KEMRI wamesema kukosa kufanikiwa kwa majaribio saba ya awali ya chanjo hiyoni funzo litakalotumiwa kufanikisha utengenezaji wa chanjo hiyo.

Vile vile taasisi hiyo imezindua mbinu mp;ya za kupima na kufanya majaribio zitakazotumiwa kutoa huduma za kmakafani katika kaunti za Kisumu na Siaya.

Hatua hiyo inakusudiwa kupunguza idadi ya vifo miongoni mwa watoto katika kaunti hizo kwa kufanya utafiti wa wA kubainisha kinachosababisha vifo vya watoto kabla ya miili yao kuzikwa.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa KEMRI Prof. Elijah Songok amesema huduma hii muhimu ni muhimu katika kuchunguza kinachosababisha vifo miongoni mwa watoto na kuvizuia.

Website | + posts
Radio Taifa
+ posts