Keir Starmer anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza baada ya chama chake cha Labour kushinda wingi wa viti katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana Alhamisi.
Starmer anatarajiwa kutwaa mikoba kutoka kwa Rishi Sunak huku chama chake cha Labour kikirejea uongozini baada ya miaka 14.
Starmer ana umri wa miaka 61. Yeye ni mwanaharakati ambaye alichaguliwa mbunge mwaka 2015 kutoka mrengo wa kushoto.
Chama cha Labour kimepata viti 410 bungeni dhidi ya viti 118 vya chama cha Conservative.