Vikosi vya ulinzi nchini KDF, vimekabidhi hospitali ya Wanini Kireri Magereza, kwa idara ya urekebishaji tabia, baada ya ujenzi wake kukamilika.
Waziri wa usalama wa taifa Prof. kithure Kindiki, alipokea hopsitali hiyo iliyo na vitanda 150, kutoka kwa mwenzake wa ulinzi Aden Duale katika taasisi ya mafunzo ya maafisa wa magereza iliyoko mtaani Ruiri, kaunti ya Kiambu.
Hospitali hiyo inajivunia kuwa na vyumba viwili vya upasuaji, kituo cha huduma za ajali na dharura, kitengo cha kujifungulia kina mama, huduma za meno na chumba cha kuhifadhi maiti miongoni mwa huduma zingine.
Akikabidhi hospitali hiyo, waziri wa ulinzi Aden Duale, alisema vikosi vya ulinzi nchini vitaendelea vitaendelea kupiga jeki idara hiyo kwa kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya kuhakikisha kituo hicho cha afya kinadumisha utoaji huduma wa ubora wa hali ya juu.
“Ufanisi huu unaashiria ushirikiano uliopo kati ya vikosi vya usalama na wizara ya usalama wa taifa, kuimarisha uwezo wetu wa kutoa huduma za afya na kuboresha umoja katika kutumikia taifa hili,” alisema waziri Duale.
Kwa upande wake, waziri wa usalama wa taifa Prof. kithure kindiki, alipongeza utaalam na ufanisi katika kukamilisha kituo hicho cha afya.
“Ushirikiano katika ya huduma ya taifa ya polisi na vikosi vya ulinzi, umefanikisha kukamilika kukamilika kwa hospitali ya huduma ya taifa ya polis ya level 4 katika barabara ya Mbagathi iliyojengwa kwa kitita cha shilingi bilioni 1.2,” alisema Prof. kindiki.
Waziri huyo alitoa hakikisho la serikali kwamba maafisa wa usalama na familia zao watapata huduma bora za afya.