Home Habari Kuu KBC yashirikiana na kaunti ya Turkana kwa sherehe za utamaduni

KBC yashirikiana na kaunti ya Turkana kwa sherehe za utamaduni

Sherehe za mwaka huu zitapeperushwa mubashara na runinga ya taifa KBC Channel 1 na Idhaa ya Kiturna inayorusha matangazo yake kupitia Idhaa ya Eastern Service.

0

Shirika la Utangazaji nchini Kenya, KBC limeshirikiana na kaunti ya Turkana katika sherehe za mwaka huu za utamaduni wa jamii ya Waturkana zitakazoandaliwa kati ya Oktoba 12 hadi 16.

Kaunti hiyo hutumia sherehe hizo kujitangaza kama eneo la kitalii na pia kuelimisha umma kuhusu mila, itikadi na utamaduni wa jamii hiyo.

Sherehe za mwaka huu zitapeperushwa mubashara na runinga ya taifa KBC Channel 1 na Idhaa ya Kiturkana inayorusha matangazo yake kupitia Idhaa ya Eastern Service.

Wakati huo huo, serikali ya kaunti ya Turkana imetenga ardhi kwa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na serikali ya kitaifa.

Idara ya nyumba ya serikali ya kaunti ya Turkana imetenga maeneo manne yatakayojengwa nyumba za gharama nafuu katika manispaa ya Lodwar.

Nyumba hizo zitajengwa katika awamu ya pili ya mradi wa KISIP2 mjini Lodwar.
Maeneo hayo yaliyobainishwa ni Soweto, Napetet, Ngitakito na Nabute ambako nyumba za kisasa zitajengwa.

Meneja wa manispaa ya Lodwar Mhandisi Benjamin Tukei alizindua ramani ya ujenzi huo na kuelezea matumaini yake kuwa nyumba hizo zitainua hadhi ya mji wa Lodwar.

Website | + posts