Shirika la utangazaji nchini KBC limenunua haki miliki za kupeperusha mubashara makala ya 31 ya michezo ya Olimpiki itakayoandaliwa jijini Paris,Ufaransa kati ya Julai 26 na Agosti 11 mwaka huu.
Wakenya watapata uhondo wa kutazama michezo hiyo kwa saa tisa kila siku na kutangazwa kupitia Idhaa zote za radio.
Kenya itashiriki katika fani sita za raga ya wanaume saba upande,Voliboli ya wanawake,,Kitwara,uogeleaji,Judo na riadha.
Mashinda hayo yatang’oa nanga tarehe 24 mwezi huu kwa mechi za makundi za soka na raga hatua ya makundi, kabla ya sherehe za kufungua michezo Julai 26.
Wanamichezo 10,500 watashindana katika fani 32 ndani ya kipindi cha majuma matatu.