Home Michezo KBC kurusha mubashara mechi za ligi ya Afrika

KBC kurusha mubashara mechi za ligi ya Afrika

0

Runinga ya taifa KBC Channel 1 itapeperusha mubashara mechi zote 14 za ligi ya mabingwa barani Afrika maarufu kama African Football League.

Pambano la ufunguzi la robo fainali litakuwa kati ya vigogo wa Tanzania Simba Sports Club ambao watakuwa nyumbani dhidi ya Al Ahly ya Misri, katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Daresalaam Tanzania.

Katika ratiba nyingine Petro Atletico ya Angola itawaalika Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini siku ya Jumamosi nao TP Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, wawaalike Esperance Tunis ya Tunisia siku ya Jumapili kabla ya Enyimba ya Nigeria kumaliza udhia na Wydad Athletic Club ya Morocco.

Mechi za marudio zitachezwa Jumatatu na Jumanne  kabla ya nusu fainali kupigwa Oktoba 29 na novemba mosi na fainali iandaliwe kati ya Novemba 5 na 11 mwaka huu.

Website | + posts