Shirika la utangazaji Kenya,KBC litarusha mubashara mechi mbili za kwanza za Kenya, kufuzu kwa fainali za kombe la bara Afrika AFCON Ijumaa hii na Jumanne ijayo.
Harambee Stars ambao wamekuwa kambini katika uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda, watawaalika Zimbabwe kesho kuanzia saa kumi alasiri, na kisha baadaye kusafiri hadi Afrika Kusini kwa mchuano wa pili wa kundi J Jumanne ijayo dhidi ya Namibia.
Mechi hizo zitapeperushwa kupitia runinga ya taifa KBC Channel 1.
Kenya imo kundi pia na Cameroon ambao watamenyana nao mwezi ujao nyumbani na ugenini.
Timu mbili bora kutoka kundi hilo zitafuzu kushiriki AFCON ya Morocco kati ya Disemba mwaka ujao na Januari mwaka 2026.