Home Habari Kuu KBC kurusha mubashara mechi mbili za Ligi Kuu kila wiki

KBC kurusha mubashara mechi mbili za Ligi Kuu kila wiki

0

Wapenzi wa kandanda nchini Kenya watapata burudani isiyo na kifani kwa kupokea mubashara mechi mbili za Ligi Kuu ya FKF kila siku ya mechi.

Kwenye mkataba uliotiwa saini siku ya Alhamisi kati ya FKF na KBC  wa kima cha shilingi milioni 240 kwa mwaka kwa miaka 7, mechi hizo zitapeperushwa kenyekenye kupitia runinga ya KBC Channel 1 na Idhaa zote 13 za shirika la KBC.

Mkataba huo ulisainiwa mbele ya Mawaziri Eliud Owalo wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali na mwenzake wa Michezo Ababu Namwamba na kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa KBC  Samuel Maina.

Michuano hiyo itaanza kupeperushwa mwishoni mwa juma hili.

 

 

Website | + posts