Home Habari Kuu Kaunti za Nyeri, Kisii, Nyamira, Kiambu na Nandi kukosa umeme leo

Kaunti za Nyeri, Kisii, Nyamira, Kiambu na Nandi kukosa umeme leo

0

Kampuni ya umeme nchini KPLC imetangaza kukatizwa kwa umeme katika kaunti 5 ambazo ni Nyeri, Kisii, Nyamira, Kiambu na Nandi leo.

Umeme katika maeneo hayo utakatizwa kati ya saa tatu asubuhi na saa 11 jioni.

Sehemu za kaunti ya Nyeri zitakazo athirika ni pamoja na Gikororo, Kahuru Mkt, Ndima T/Factory, Kiaruhiu, Gathaithi, Mathia, Canteen, Gitangaruri, Ndima Kanini, Kahuro TBC, Ndiriti, Kiang’ombe, Gathambi, Muragara, Kanyai TBC, Kiambagathi, Mihuru TBC na Mununga.

Katika kaunti ya Kiambu maeneo ya Ngethu Water Works Upper Camp, Gathugu, Kagonye, Kiriko Mission, Kariminu Dam, Kanyoni, Ndiko, Gakoe, Thuraku, Mwimuto, Gachege, Njahi, Karatu, Karinga, Gitwe, Wanugu, Ndarugu, Gacharage Water na Kirangi yatakosa umeme.

Huko Nyamira sehemu zitakazokatiziwa umeme ni Manga, Ritongo, Juvenile, Manga Sengera, Nyaisa na mengine ya karibu.

Na katika kaunti ya Nandi sehemu kama KCC Lessos, Emdin, Terige, Kapnyeberai na Kilibwoni hazitakuwa na umeme sawa na sehemu mbali mbali za kaunti ya Kisii.

Website | + posts