Home Kaunti Kaunti ya Makueni kuanzisha mpango wa afya ya wanyama na ufugaji

Kaunti ya Makueni kuanzisha mpango wa afya ya wanyama na ufugaji

0
kra

Kaunti ya Makueni imechaguliwa na serikali ya kitaifa kuongoza mpango wa kitaifa wa afya ya wanyama na ufugaji.

Mpango huo unanuia kuimarisha afya ya mifugo kupitia kampeni kamili za chanjo na kukuza ufugaji bora.

kra

Uteuzi wa Makueni ni uthibitisho wa utendakazi wake wa kupigiwa mfano katika kuendesha kampeni za kila mwaka za chanjo, sehemu muhimu ya mkakati wake mpana wa kukabiliana na magonjwa ya mifugo.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kaunti ya Makueni imefanikiwa kuchanja zaidi ya mifugo 400,000 wakiwemo ng’ombe, kondoo na mbuzi.

Chanjo hizo zimelenga magonjwa kama vile ugonjwa wa ngozi wa Lumpy, homa ya Bonde la Ufa na ugonjwa wa kuambukiza wa Caprine Pleuropneumonia miongoni mwa mengine.

Mpango huo utatumika kama kielelezo kwa kaunti zingine, ukionyesha mbinu mwafaka za kuboresha afya ya mifugo na tija kupitia chanjo ya utaratibu na mbinu bora za kuzaliana.