Serikali ya kaunti ya Kwale imetoa hundi ya shilingi milioni 41, kufadhili elimu kwa wanafunzi wa shule za upili katika wadi 14, ambazo hazikuwa zimepata ufadhili huo.
Akizungumza wakati wa kutoa fedha hizo kwa wanafunzi wa Wadi za Bongwe-Gombato, Ukunda na Kinondo huko Msambweni, Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani, alisema kuwa licha ya bajeti za kaunti kupunguzwa kutokana na kuondolewa kwa mswada wa fedha wa mwaka 2024/2025 ,serikali yake haitaondoa hazina ya ufadhili wa elimu.
Achani alisema ufadhili huo wa shilingi milioni 500, utahakikisha wanafunzi kutoka kaunti ya kwale hawasalii nyumbani kwa sababu ya ukosefu wa karo.
Wazazi na wanafunzi wali toa wito kwa serikali ya kaunti ya Kwale, kuendeleza mpango wa ufadhili wa elimu ili kupiga jeki sekta ya elimu kwale.