Home Kaunti Kaunti ya kilifi yalalamika kuhusu miili ya Shakahola ambayo haijachukuliwa

Kaunti ya kilifi yalalamika kuhusu miili ya Shakahola ambayo haijachukuliwa

Takriban mili 429 haijachukuliwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Malindi.

0

Serikali ya Kaunti ya Kilifi, imetishia kuihamisha takriban mili 100 ya waathiriwa wa matukio ya Shakahola ambayo haijachukuliwa na jamaa zao katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Kaunti hiyo, hadi hospitali ya kitaifa ya Kenyatta.

Takriban mili 429 haijachukuliwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Malindi.

Huku miili kadhaa ikitambuliwa na kuchukuliwa na jamaa zao, idadi kubwa ya miili iliyofukuliwa kutoka msitu wa shakahola, ingali haijachukuliwa.

Gavana wa Kaunti hiyo Gideon Mung’aro amesema, hali hiyo si mzigo tu kwa Kaunti husika bali pia imechangia uvundo unaowaathiri wakazi.

Gavana Mung’aro aliyezungumza huko Magarini, walipokuwa wakikabidhi misaada ya vyakula, kwa waathiriwa wa mafuriko, aliishauri serikali kuu iingilie kati sula hilo.

Alipoizuru Kaunti ya Kilifi mwezi Machi mwaka huu, waziri wa usalama wa kitaifa Profesa Kithure Kindiki, alisema, serikali ingeisadia Kaunti hiyo kulipa bili za hifadhi hizo.