Home Kaunti Kaunti ya Kericho yapokea vifaa vya matibabu kutoka KEMSA

Kaunti ya Kericho yapokea vifaa vya matibabu kutoka KEMSA

Kulingana na Mutai, vifaa hivyo vya matibabu vinatosha kudumu kwa muda wa miezi mitatu katika vituo vya afya.

0
Hospitali katika kaunti ya Kericho, kupokea vifaa vya matibabu.

Halmashauri ya kusambaza vifaa vya matibabu nchini (KEMSA), imeanza kusambaza vifaa vya matibabu vya thamani ya shilingi milioni 70 kwa vituo vya matibabu kaunti ya Kericho.

Wakati wa sherehe ya uzinduzi wa zoezi hilo, Gavana wa kaunti ya Kericho Dkt. Eric Mutai, alisema serikali ya kaunti yake inajizatiti kutoa huduma bora za afya kwa wakazi wa eneo hilo, kupitia kutoa vifaa vya matibabu katika vituo vya afya.

Kulingana na Mutai, vifaa hivyo vya matibabu vinatosha kudumu kwa muda wa miezi mitatu katika vituo vya afya.

Akizungumza na wanahabari katika hospitali ya rufaa ya Kericho, Gavana huyo alisema serikali ya kaunti hiyo kwa ushirikiano na serikali ya kitaifa, imewaajiri wahamasishaji 1600 wa afya ya jamii.

Aidha Mutai alisema hospitali ya rufaa ya Kericho, imepandishwa ngazi hadi level 5 na itaanza kutoa huduma zake katika ngazi hiyo kuanzia tarehe 20 mwezi Oktoba.

“Tuna wahudumu wa afya ambao wana ujuzi na wamepokea mafunzo kuhusu kushughulikia ugonjwa wa saratani,” alisema Gavana huyo.

Website | + posts