Home Habari Kuu Kaunti sita kukosa umeme Alhamisi yasema KPLC

Kaunti sita kukosa umeme Alhamisi yasema KPLC

0

Kampuni ya usambazaji umeme nchini KPLC imetangaza kukosekana kwa nguvu za umeme katika kaunti sita siku ya Alhamisi.

Usumbufu huo utatokea kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni katika maeneo kadhaa ya kaunti hizo.

Maeneo yatakayoathirika katika kaunti ya Nairobi ni pamoja na Saika,Langata,Mombasa Riad na GSU.

Kaunti nyingine zitakazokabiliwa na usumbufu huo ni Nyeri,Kajiado,Kiambu,Machakos na Kirinyaga.

Hata hivyo KPLC haijatoa sababu zote za kuchangia kukosekana kwa nguvu za umeme.