Home Habari Kuu Kaunti nane kukosa umeme, yasema KPLC

Kaunti nane kukosa umeme, yasema KPLC

0

Kaunti nane nchini zitakosa umeme leo Alhamisi, Septemba 28, 2023.

Kwa mujibu wa kampuni ya umeme, KPLC, kaunti zitakazoathirika ni pamoja na Nairobi, Kilifi, Trans Nzoia, West Pokot, Kisumu, Migori, Embu, Isiolo na Kiambu.

Maeneo ya kaunti ya Nairobi yatakayokabiliwa na usumbufu huo ni kama vile Muthaiga Road, Muthaiga Crescent, Naivasha Avenue na Tchui.

Maeneo mengine ni Serengeti, Mutundu Road, Mua Park, Gertrude Hospital, Saika, Umoja 3, baadhi ya maeneo ya Kangundo Road, Obama, KPCU, Silanga, Slaughter House, Maili Saba, Kayole Junction na mengineyo.

Website | + posts