Mgao wa mapato wa shilingi bilioni 32 wa mwezi huu kwa kaunti utatolewa leo Alhamisi.
Rais William Ruto anasema shilingi bilioni 2.3 za mwezi Julai zitatolewa kwa watu wote wanaonufaika na fedha zinazotolewa chini ya mpango wa uhifadhi wa jamii kote nchini.
Rais aliyasema hayo akiwa katika kaunti ya Lamu wakati akianza ziara ya siku tano katika eneo la Pwani kuanzia leo Alhamisi.
“Niliahidi kwamba hakuna namna tunavyoweza kujilipa mishahara kabla ya kuwalipa watu wanaodhuriwa,“ alisema Rais Ruto.
Wazee, watu wenye ulemavu na watoto mayatima wanafaidika chini ya mpango wa uhifadhi wa jamii maarufu kama Inua Jamii.
Wakati wa ziara yake katika eneo la Pwani, Rais atazuruu kaunti za Lamu, Kilifi, Mombasa, Kwale na Tana River.
Rais atazindua na kukagua miradi mbalimbali ya serikali inayowanufaisha raia wa kawaida wakati wa zaiara hiyo.