Home Habari Kuu Kaunti 5 zaathiriwa na ukosefu wa umeme leo

Kaunti 5 zaathiriwa na ukosefu wa umeme leo

0

Kampuni ya huduma za umeme nchini KPLC ilitoa notisi kwa wateja wake kuhusu kukatizwa kwa umeme katika sehemu za kaunti tano humu nchini.

Kaunti hizo ni Nairobi, Kilifi, Kwale, Uasin Gishu na Kisumu na hali hiyo itadumu kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni leo Jumapili.

Huko Kilifi maeneo yaliyoathirika ni pamoja na Ahadi Beach, Marina Mtwapa, Kanamai Timboni, Sultan na Kwa Jeki,

Katika kaunti ya Nairobi mitaa ya Tena, Rockfield, Umoja na mingine iliyo karibu na barabara ya Outering itakosa huduma za umeme.

Maeneo ya Msambweni, Sawasawa na Viungujini katika kaunti ya Kwale yatakosa stima mchana wa leo na huko Kisumu hakutakuwa na stima katika maeneo kama vile Bandani.

Kampuni hiyo ya KPLC ilielezea kwamba kukatizwa kwa umeme katika maeneo hayo kunanuiwa kutoa fursa ya kuboresha mifumo yake.

Website | + posts