Home Kimataifa Kanja: Nitahakikisha maafisa wote wa polisi wanawajibika

Kanja: Nitahakikisha maafisa wote wa polisi wanawajibika

Aidha Kanja alidokeza kuwa atashirikiana na asasi zingine za usalama, ili kuangamiza ujangili katika eneo la North Rift, kupitia kuwawezesha polisi wa akiba.

0
Douglas Kanja, alipeyendekezwa kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi.
kra

Dougla Kanja aliyependekezwa kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi, ameahidi  kuhakikisha kuwa maafisa wa polisi wanawajibika na kuboresha utendakazi katika vituo vya polisi iwapo bunge litamuidhinisha.

Alipofika mbele ya kamati ya bunge la taifa kuhusu utawala na usalama wa kitaifa, na kamati ya bunge la Seneti  kuhusu usalama wa taifa, ulinzi na mambo ya nje, Kanja  alisema atafanya kazi kwa karibu na tume ya huduma ya polisi, ili kuboresha maslahi ya maafisa wa polisi na pia kuangazia baadhi ya masuala yanayoathiri utendakazi wao kama vile mafunzo,na kupandishwa vyeo miongoni mwa masuala mengine.

kra

Aidha Kanja alidokeza kuwa atashirikiana na asasi zingine za usalama, ili kuangamiza ujangili katika eneo la North Rift, kupitia kuwawezesha polisi wa akiba.

Wabunge hao walimtaka Kanja awaeleze mikakati atakayotumia kuimarisha uhusiano kati ya maafisa wa polisi, idara ya Ujasusi nchini NIS, na idara ya uchunguzi wa makosa ya jinai DCI.

Pia wabunge hao walichunguza jukumu ambalo Kanja alitekeleza alipokuwa naibu inspekta jenerali wa polisi, wakati wa maandamano ya hivi majuzi dhidi ya serikali.

Alisema kwamba iwapo ataidhinishwa na bunge, ataweka mikakati kuimarisha ulinzi katika afisi za serikali,hasa wakati wa maandamano.