Home Taifa Kanisa latakiwa kubuni fursa kwa kina mama na vijana

Kanisa latakiwa kubuni fursa kwa kina mama na vijana

0
kra

Mama Taifa Rachel Ruto, ameitaka kanisa na mashirika mengine ya kidini kushirikiana na serikali kuunda fursa za ajira kwa wanawake na vijana humu nchini.

Bi. Rachel Ruto aliyasema hayo alipohudhuria maadhimisho ya miaka kumi ya kanisa la “Gospel Embassy Chapel” mjini Kisii katika kaunti ya Kisii.

kra

Mkewe Rais alisifia mpango wa kuwezesha washiriki wa kanisa hilo almaarufu “Member Empowerment Program” unaoendeshwa na kanisa ambapo kina mama na vijana wasiokuwa na ajira wanapatiwa mtaji wa kuanzisha biashara.

Awali kanisa hilo lilianzisha kiwanda cha kuunda viatu vya ngozi vya wanafunzi wa shule ambapo washiriki wapatao 20 wamepata ajira ya kudumu.

Racheal alitaka makanisa na mashirika ya kidini kutekeleza pia jukumu muhimu la kujuza vijana kuhusu fursa mbali mbali zinazotolewa na serikali.

Alitaja mpango wa serikali wa ufadhili wa elimu ya juu unaolenga wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za mafunzo ya kiufundi uliozinduliwa na wizara ya elimu hivi maajuzi.

Mama Rachel Ruto alihutubia pia wanafunzi wa shule ya upili ya wavulana ya Kisii ambapo aliungana na jamii nzima ya shule hiyo kuomboleza kifo cha mmoja wao.

Sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya kanisa la Gospel Assembly Chapel zilihudhuriwa na viongozi kadhaa wa kidini akiwemo mhubiri Mark Kariuki na waimbaji wa nyimbo za injili bila kusahau mwanzilishi wa kanisa hilo mhubiri Peter Morwabe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here