Home Michezo Kandie Kibiwott kujaribu bahati tena Valencia

Kandie Kibiwott kujaribu bahati tena Valencia

0

Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za nusu marathoni  Kandie Kibiwott  na Joan Chelimo,ni miongoni mwa Wakenya watakaojitosa nchini Uhispania Jumapili hii kutimka mbio za Valencia Marathon.

Kibiwott atakuwa akitimka marathon ya  pili baada ya kukamilisha mbio za Newyork City marathon mwaka huu.

Hata hivyo atakabiliwa na upinzani kutioka kwa bingwa mara tatu wa Olimpiki Kenenisa Bekele wa Ethiopia , Gabriel Geay  wa Tanzania aliyemaliza wa pili katika mashindano ya London marathon mwaka huu na Mganda Joshua Cheptegei, atakayeshiriki marathon kwa mara ya kwanza.

Wakenya wengine watakaoshiriki Jumapili ni Alexander Mutiso, na  Titus Kipruto.

Mbio za wanawake zitamshirikisha  Joan Chelimo atakayepambana na Tsegay Gemechu,Almaz Ayana,Worknesh Degefa na  Hiwot Gebrekidan wote kutoka Ethiopia.

Website | + posts