Home Biashara Kampuni za uchukuzi wa mizigo zatakiwa kuwa na idhini ya CA

Kampuni za uchukuzi wa mizigo zatakiwa kuwa na idhini ya CA

Mugonyi alidokeza kuwa tovuti ya CA, imeorodhesha kampuni ambazo zimeidhinishwa kutoa huduma za uchukuzi wa mizigo.

0

Magari ya uchukuzi wa umma na kampuni zinazotoa huduma za uchukuzi wa mizigo bila leseni kutoka halmashauri ya mawasiliano nchini CA,  zimeonywa kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yazo.

Mkurugenzi Mkuu wa halmashauri ya mawasiliano nchini David Mugonyi, alitoa ilani iliyosema kampuni za uchukuzi wa mizigo zinazoendesha biashara hiyo bila leseni ya CA, ni ukiukaji wa sheria.

“Halmashauri hii imegundua kuwa baadhi ya magari ya uchukuzi wa umma, yanatoa huduma za uchukuzi wa mizogo bila idhini kutoka kwa halmashaurinya CA,” ilisema halmashauri hiyo.

Mugonyi aliwahimiza wananchi kutumia posta au kampuni za uchukuzi ambazo zimesajiliwa ili kuhakikisha usalama wa mali yao, na pia kupunguza hatari zinazotokana na kutumia kampuni ambazo hazijaidhinishwa.

Mugonyi alidokeza kuwa tovuti ya CA, imeorodhesha kampuni ambazo zimeidhinishwa kutoa huduma za uchukuzi wa mizigo.

Hatua hiyo inajiri baada ya halmashauri ya mawasiliano nchini CA, kuchapisha kwenye gazeti rasmi la serikali mapema mwezi Aprili, ilani kwa kampuni sita za uchukuzi wa mizigo, kuwa leseni zao zitafutiliwa mbali baada ya kukamilika kwa ilani hiyo.

Kufikia mwezi Juni mwaka 2021, kampuni 289 za uchukuzi wa mizigo zilikuwa zimesajiliwahapa nchini.

Website | + posts