Home Habari Kuu Kampuni za mabawabu zapewa makataa kurejesha stakabadhi za waajiriwa

Kampuni za mabawabu zapewa makataa kurejesha stakabadhi za waajiriwa

0

Kampuni zote za kibinafsi za mabawabu nchini zimepewa makataa ya saa 48, kurejesha stakabadhi zote za wafanyikazi wao la sivyo zichukuliwe hatua kali za kisheria.

Mamamlaka inayothibiti kampuni za kibinafsi za usalama nchini  PSRA, kwenye ilani iliyotolewa Jumatano imesema ni kinyume cha sheria kwa kampuni hizo kukatalia stakabadhi za wafanyikazi wao kama vile vyeti vya masomo  na vitambulisho .

Kulingana na sheria za mwaka 2016,PSRA imepewa mamlaka ya kuzipokonya kampani za ulinzi leseni za kuhudumu iwapo zitakiuka sheria zilizowekwa.

Mkurugenzi Mkuu wa PSRA Mohammed Fazul amesema wenye kampuni za kibinafsi za ulinzi ambao hawatazingatia agizo hilo watachukuliwa hatua za kisheria.

Wafanyikazi ambao stakabadhi zao zilichukuliwa na waajiri wao wametakiwa kupiga ripoti mara moja kwa kupitia nambari ya WhatsApp +254 799 429 001 au kupitia barua pepe kwa ; complaints@psra.go.ke.

Haya yanajiri siku chache baada ya serikali kuanzisha shughuli ya kusajili mabawabu kote nchini huku pia ikiweka kiwango cha chini cha mshahara kuwa shilingi 30,000 kwa kila bawabu.

Website | + posts