Home Michezo Nike yazindua uzi mpya wa Kenya wa Olimpiki

Nike yazindua uzi mpya wa Kenya wa Olimpiki

0

Kampuni ya Marekani Nike imezindua sare mpya itakayotumiwa na wanariadha wa Kenya kwenye makala ya 33, ya michezo ya Olimpiki  jijini Paris Ufaransa.

Hafla hiyo iliandaliwa Alhamisi usiku nchini Ufaransa, takriban siku 105 kabla ya kung’oa nanga kwa michezo ya Olimpiki  Julai 26 hadi Agosti 11.

Uzi huo mpya utachukua nafasi ya ule wa awali ambao umetumika kwa makala ya mwaka 2016 na 2020 ya Olimpiki.

Bingwa wa Olimpiki  katika mbio za mita 1500 Faith Kipyegon na bingwa  wa Olimpiki wa marathon  Eliud Kipchoge walihudhuria hafla hiyo.